Taarifa ya Awali:

Wakazi wa Himo wapo katika kituo cha Polisi himo ambapo gari la Shule ya Scolastica limekamatwa na mabosi ya kura nyingine 3 zilizokua zinasafirishwa na pikipiki na nyingne 3 zilizokamatwa na James Mbatia zimefikishwa Kituo cha Polisi Himo.

Tayari watu niwengi sana eneo hili tukiongozwa na Mbatia anayesubiri kuapishwa na Mrema waliokuja kushuhudia.

UPDATE 1:


UPDATE 2:

Muda huu Mbatia katoka nje akiwa na Mrema na kuwahamasiha wananchi watoke barabarani na wakae pembeni na waendelee kushangilia kama ndo wanachotaka. Wamesema kuwa wanawasubiri NEC kuja kukagua na mzee Mrema baada ya kukataliwa na wananchi akaamua kutumia salamu ya CHADEMA na UKAWA ya "peeepoozi" ila kesho wahakikishe wanaenda kupiga kura

UPDATE 3:
Kwa mujibu wa RPC Kilimanjaro, imedaiwa kuwa katika jimbo la Vunjo kuna wasimamizi wa vituo viwili walionekana na masanduku ya kupigia kura wakiwa wanakwenda vituoni kwao huko maeneo ya Himo na Marangu; Baadhi ya wananchi waliwatilia mashaka na kuwakamata usiku na kuwafikisha kituoni na masanduku yao yakiwa salama; anasubiriwa Mkurugenzi wa Moshi vijijini awatambue.