Tuesday, 27 October 2015

Matokeo Ya Urais: Dk Magufuli anaongoza Majimbo 17, Lowassa Majimbo 10

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Usiku huu imeendelea kutoa matokeo ya awali ya urais katika majimbo 27 ambapo mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli anaongoza kwa majimbo 17 wakati Mgombea wa Chadema, Edward Lowassa anaongoza majimbo 10.

Matokeo hayo yametangazwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Damian Lubuva kwa awamu tatu, ambapo asubuhi  mwenyekiti huyo alitangaza majimbo matatu ambayo ni  Paje, Makunduchi na Lulindi ambayo yote Dk Magufuli ameongoza.
 
Majira ya alasiri , Jaji Lubuva alitangaza majimbo mengine 10 ambapo kati ya hayo majimbo sita yalionyesha Dk.Magufuli anaongoza huku majimbo manne yakionyesha Lowassa anaongoza.

Usiku  huu  majira  ya  saa  mbili , Jaji Lubuva ametangaza majimbo mengine 14 ambapo kati ya hayo majimbo 8 yalionyesha Dk.Magufuli anaongoza huku majimbo 6 yakionyesha Lowassa anaongoza.
 
Majimbo hayo ni kama  ifuatavyo:
Matokeo ya Urais Singida Mjini
Kura: 56,558 
Magufuli (CCM): 36,035 
Edward Lowassa (Chadema): 19,007

Matokeo ya Urais Jimbo la Lindi Mjini 
Kura: 38,992 
Magufuli (CCM): 21,088 
Edward Lowassa(Chadema): 17,607 

Matokeo ya Urais Jimbo la Njombe Mjini 
Kura: 55,772 
Magufuli (CCM): 33,626 
Edward Lowassa(Chadema):20,368

Matokeo ya Urais Jimbo la Peramiho 
Kura:45,374 
Magufuli (CCM): 32,505 
Edward Lowassa (Chadema): 11,291

Matokeo ya Urais Jimbo la Mkinga 
Kura: 39,788 
Magufuli (CCM): 23,798 
Edward Lowassa (Chadema): 15,142

Matokeo ya Urais Jimbo la Moshi Mjini 
Kura:79,814 
Magufuli (CCM): 28,909
Edward Lowassa (Chadema): 49,379

Matokeo ya Urais Jimbo la Nanyamba 
Kura: 44,437 
Magufuli (CCM): 24,904 
Edward Lowassa (Chadema): 16,992

Matokeo ya Urais Jimbo la Mbinga Mjini 
Kura: 42,717
Magufuli (CCM): 29,295 
Edward Lowassa (Chadema):11,695

Matokeo ya Urais Jimbo la Kisarawe 
Kura: 38,012 
Magufuli (CCM): 24,086
Edward Lowassa (Chadema): 13,093

Matokeo ya Urais Jimbo la Mgogoni 
Kura: 7,539 
Magufuli(CCM):710 
Edward Lowassa (Chadema): 6,506

Matokeo ya Urais Jimbo la Mtambwe 
Kura: 7,620 
Magufuli (CCM): 428 
Edward Lowassa (Chadema): 6,937

Jaji Lubuva amesema kuwa matokeo ya majimbo mengine ambayo yatakuwa tayari yatatolewa kesho  saa  tatu  asubuhi.

Matokeo  Yaliyotangazwa mchana Yako  Hapo  Chini. Bonyeza  Picha  Kuyaona  Vizuri

Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *