Wednesday, 28 October 2015

MATOKEO YA AWALI KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KOZI YA MUHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII


INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 
MATOKEO YA AWALI KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KOZI YA
MUHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kujiunga na kozi ya Muhudumu wa afya ngazi ya jamii (Community Health) kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kuwa, Uteuzi wa awali umefanyika na waombaji 3985 kati ya 9797 wameteuliwa kujiunga na vyuo mbalimbali. Matokeo ya uteuzi huo yanapatikana katika kurasa binafsi (Profiles) za waombaji

Waombaji wote ambao wamechaguliwa katika awamu hii wanapaswa kuthibitisha kuwa wataripoti katika vyuo walivyopangiwa na mwisho wa kuthibitidha ni Ijumaa tarehe 04 November 2015. Iwapo muombaji hatathibitisha, nafasi hiyo itatolewa kwa mwingine. Kuweza kuthibitisha bonyeza hapa au ingia katika ukurasa wako binafsi (Profile) kudhibitisha.

Kwa wale ambao bado hawajapangiwa vyuo, kurasa binafsi zenu zina maelezo yenye sababu za kutopangiwa chuo katika awamu hii na maelekezo ambayo unatakiwa kuyatekeleza ili mfumo utakapochakata uteuzi wa awamu nyingine siku ya Jumatatu 05 November 2015 idadi kubwa zaidi ya waombaji iweze kupangiwa vyuo katika nafasi 278 zilizobaki wazi.
 
Imetolewa na:
Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
28 October 2015
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *