HAYA HAPA MATOKEO YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO VYA UALIMU-KUPITIA NACTE 2015/2016 | MASWAYETU BLOG
Breaking News
Loading...
Millionaire  Ads

Wednesday, 21 October 2015

HAYA HAPA MATOKEO YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO VYA UALIMU-KUPITIA NACTE 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

 1. Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kujiunga na kozi mbalimbali za Ualimu kwa ngazi ya Stashahada na Stashahada ya Juu kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kuwa, Kikao cha Pamoja cha Udahili (Joint Admission Committee on Teachers Education) kilichofanyika tarehe 15 Oktober 2015 na kukutanisha Uwakilishi wa Wizara, Baraza (NACTE), wakuu wa vyuo vinavyotoa Mafunzo ya Ualimu na wadau wengine washiriki kiliidhinisha uteuzi wa awali ambapo waombaji 8544 kati ya 14470 wameteuliwa kujiunga na vyuo mbalimbali.

 1. Matokeo ya uteuzi huo yanapatikana katika kurasa binafsi (Profiles) za waombaji na pia yatatangazwa moja kwa moja na vyuo husika kwa wale waliopitia kwenye “institutional panels”. Matokeo ya jumla yanapatikana pia katika tovuti ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (www.nacte.go.tz)

 1. Waombaji wote ambao wamechaguliwa katika awamu hii wanapaswa kuthibitisha kuwa wataripoti katika vyuo walivyopangiwa na mwisho wa kuthibitidha ni Ijumaa tarehe 30 Oktoba 2015. Iwapo muombaji hatathibitisha, nafasi hiyo itatolewa kwa mwingine.

 1. Kwa wale ambao bado hawajapangiwa vyuo, kurasa binafsi zenu zina maelezo yenye sababu za kutopangiwa chuo katika awamu hii na maelekezo ambayo unatakiwa kuyatekeleza ili mfumo utakapochakata uteuzi wa awamu ya pili siku ya Jumatatu 26 Oktoba 2015 idadi kubwa zaidi ya waombaji iweze kupangiwa vyuo kwani hadi sasa nafasi zipatazo 14548 hazijajazwa.
Imetolewa na:
Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu yaUfundi (NACTE)
20 Oktoba 2015
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APPLICATION MPYA YA MASWAYETU BLOG

google+

linkedin

About Author
 • Donec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Sed posuere consecteturDonec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Read More

  0 comments:

   

  About Us