Friday, 11 September 2015

VIJANA WA MUJIBU 2,909 JKT WAFUNGA MAFUNZO YAO-KIKOSI CHA RUVU PWANI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
2,909 Wahitimu Mafunzo JKT Operesheni Kikwete

2,909 Wahitimu Mafunzo JKT Operesheni Kikwete

Vijana 2,909 wa mujibu wa sheria waliojiunga na Jeshi la Kujenga Taifa Operesheni Kikwete wamehitimu mafunzo yao ya miezi mitatu katika kikosi cha Ruvu-JKT. Kati ya vijana hao, 1,993 ni wavulana na 916 ni wasichana. Katika sherehe fupi iliyofanyika katika viwanja vya kambi ya Ruvu-JKT, Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Eng Evarist Ndikilo alifunga Mafunzo hayo ya vijana waliomaliza kidato cha sita yanayoendeshwa kwa lengo la kuwafundisha Uzalendo na elimu ya kujitegemea.
Akiongea katika sherehe hizo, Mkuu wa Mkoa aliwataka vijana waliohudhuria mafunzo hayo kuwa wazalendo wa nchi yao hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu kwani wanapaswa kutumia vyema mafunzo walioyapata katika kulijengea sifa JKT kwa mafunzo bora kwa vijana wote wa kitanzania bila ya kujali makabila yao, dini zao, jinsia zao na itikadi zao.
Wakisoma Risala kwa Mgeni rasmi, Vijana wahitimu walimueleza kuwa muda wa mafunzo uongezwe kutoka miezi mitatu hadi sita, kwani wakifanya hivyo wataongeza ari ya vijana kujifunza zaidi elimu ya uzalendo kwa Taifa lao.
Naye mkuu wa Utawala na Mafunzo wa JKT, Brigedia Jenerali Jacob Kingu alimueleza Mgeni rasmi kuwa mafunzo hayo ya vijana wa mujibu wa sheria yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika Serikali ya awamu ya nne. Tangu kurejeshwa mafunzo hayo mwaka 2013 hadi sasa takribani vijana 67,000 wameweza kuhudhuria mafunzo kwa ufanisi.
Akimshukuru Mgeni Rasmi, Mkuu wa kikosi cha Ruvu-JKT, Luteni Kanali Charles Mbuge alimkabidhi Mkuu wa Mkoa vifaranga vya kuku wa kienyeji 500 kwa ajili ya vikundi vya kina Mama wa Mkoa wa Pwani katika kuboresha Maisha bora kwa kila Mtanzania. Sherehe hizo ziliburudishwa na vikundi mbalimbali vya sanaa na muziki kutoka kambi ya Ruvu-JKT.
Sambamba na ufungwaji huo Ruvu JKT, sherehe za kuhitimu mafunzo hayo zilijumuisha pia kambi ya Makutopora – Dodoma, Mafinga – Iringa, na Bulombora – Kigoma. Mafunzo hayo yaliyoanza mapema Mwezi Juni, 2015 katika jumla ya kambi 10 za mafunzo za JKT nchini kote, yanategemea kufungwa katika kambi zilizosalia kati ya tarehe 09 (Mgambo – Tanga na Msange – Tabora); tarehe 12 Septemba, 2015 (Kanebwa na Mtabila – Kigoma), na hivyo kuwapa wahitimu muda wa kwenda kufanya maandalizi ya kujiunga na vyuo ya elimu ya juu kote Nchini.


Wahitimu wa Mafunzo kwa Mujibu wa Sheria  wakila kiapo cha utii.

Wahitimu wa Mafunzo kwa Mujibu wa Sheria wakila kiapo cha utii.

Wahitimu wa Mafunzo kwa mujibu wa Sheria wakipita mbele ya mgeni Rasmi

Wahitimu wa Mafunzo kwa mujibu wa Sheria wakipita mbele ya mgeni Rasmi

 

Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *