Tuesday, 25 August 2015

MH.LAURANCE MASHA AKAMATWA NA JESHI LA POLISI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Aliyekuwa waziri wa Mashauri ya Ndani ambae sasa ni mwanachama wa CHADEMA Mh Laurance Masha amekamatwa jioni ya leo na jeshi la polisi nchini.

Tukio la kukamatwa Masha limefuatia kukamatwa kwa wanachama 18 waliokuwa kwenye harakati za kawaida za uenezi wa chama chao katika kampeni ya kawaida ya nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu ambayo haizuiwi na sheria yoyote ile nchini.

Baada ya kukamatwa vijana hao na kufikishwa kituo cha Ostarbay, Mh Masha aliamua kwenda kufuatilia sababu za kukamatwa kwa wanaukombozi hao, ajabu alipofika tu nae akatiwa mbaroni.
Post a Comment

Our Team

Video of the Day

Contact us

Name

Email *

Message *